KITENGO CHA UKAGUZI WA NDANI
• Kitengo cha Ukaguzi wa ndani ni moja ya vitengo vya kudumu katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe.
• Kitengo kinafanya ukaguzi wa Idara na vitengo vyote vya Halmashauri na kuziwasilisha kwa Mkurugenzi Mtendaji(W),Kamati ya ukaguzi,RAS,NAO na IAG.Taarifa hizi huandaliwa na kuwasilishwa kila robo mwaka.
• Hata hivyo kitengo kinaweza kutoa ushauri pale utakapohitajika na kufanya ukaguzi maalumu kwa maagizo ya Mkurugenzi Mtendaji(W)
• Kitengo kinafanya kazi kwa kuzingatia Miongozo na sheria mbalimbali kama ifuatavyo;
• Public Finance Act no 6 revised 2004 with its regulations.
• Public procurement Act 2004 with its regulations 2005.
• Public scheme of service.
• Public service Act 2002 and its regulation 2003.
• IPPF.
• LAPF 2009.
• Hoja na Maagizo yote ya kisheria.
IDADI YA WATUMISHI KATIKA KITENGO
Kitengo kina idadi ya Watumishi wanne(4) ambao wote wapo Makao Makuu ya Wilaya.
SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA KITENGO
• Kuandaa Mpango kazi wa kila mwaka.
• Kufanya ukaguzi kwa Idara na vitengo vyote kama ilivyoainishwa katika mpango kazi.
• Kutoa ushauri kwa Mkurugenzi Mtendaji(W) kuhusu mfumo wa udhibiti wa ndani na ukaguzi wa nje.
• Kuandaa taarifa ya kila robo mwaka na kuiwasilisha kwa Mkurugenzi Mtendaji(W),Mkaguzi wa nje,RAS na Mkaguzi Mkuu wa ndani wa serikali(IAG).
• Kufanya kazi nyinginezo kwa maagizo ya Mkurugenzi Mtendaji.
Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.